Unapohisi Uvivu
Qurani na Hadithi · Kiarabu · Matamshi · Maana · Sauti
Ni dua zipi zinaweza kusaidia unapohisi uvivu?
Ukurasa huu unakusanya dua 4 za kukusaidia kukabiliana na hisia hii. Kila dua ina maandishi ya asili ya Kiarabu, matamshi yanayosomeka, maana yake kwa Kiswahili na rejeo la Qurani au Hadithi inapopatikana. Tumia kitufe cha sauti ikiwa rekodi ipo.
اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْجُبْنِ وَالْبُخْلِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ وَقَهْرِ الرِّجَالِ
Allāhumma innī aʿūdhu bika min-l-hammi wa-l-ḥazan, wa aʿūdhu bika min-l-ʿajzi wa-l-kasal, wa aʿūdhu bika min-l-jubni wa-l-bukhl, wa aʿūdhu bika min ghalabati-d-dayni wa qahri-r-rijāl.
Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni, kutoweza na uvivu, ubakhili na uwoga, uzito wa deni na kushindwa na watu.
— (Abū Dāwūd 1555)
يَا حَيُّ يَا قَيُّوْمُ ، بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيْثُ ، أَصْلِحْ لِيْ شَأْنِيْ كُلَّهُ ، وَلَا تَكِلْنِيْ إِلَىٰ نَفْسِيْ طَرْفَةَ عَيْنٍ
Yā Ḥayyu yā Qayyūm, bi-raḥmatika astaghīth, aṣliḥ lī sha’nī kullah, wa lā takilnī ilā nafsī ṭarfata ʿayn.
Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu yote, wala usiniachie mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia), hata kwa muda (mdogo, kama muda) wa kupepesa jicho.
— (Nasā’ī in ʿAmal al-Yawm wa-l-Laylah 570)
اَللّٰهُمَّ إِنّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْبُخْلِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْجُبْنِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ أَنْ أُرَدَّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الدُّنْيَا ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ
Allāhumma innī aʿūdhu bika mina-l-bukhl, wa aʿūdhu bika mina-l-jubn, wa aʿūdhu bika an uradda ilā ardhali-l-ʿumur, wa aʿūdhu bika min fitnati-d-dunyā, wa aʿūdhu bika min ʿadhābi-l-qabr.
Ewe Mwenyezi Mungu najilinda kwako kutokana na ubakhili, na ninajilinda kwako kutokana na uwoga, na ninajilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na ninajilinda kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi.
— (Bukhārī 6370)
اَللّٰهُمَّ عَافِنِيْ فِيْ بَدَنِيْ ، اَللّٰهُمَّ عَافِنِيْ فِيْ سَمْعِيْ ، اَللّٰهُمَّ عَافِنِيْ فِيْ بَصَرِيْ ، لَا إِلٰهَ إِلَّا أَنْتَ ، اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنَ الْكُفْرِ وَالْفَقْرِ، وأَعُوْذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، لَا إِلٰهَ إِلَّا أَنْتَ
Allāhumma ʿāfinī fī badanī, Allāhumma ʿāfinī fī samʿī, Allāhumma ʿāfinī fī baṣarī, lā ilāha illā Ant, Allāhumma innī aʿūdhu bika mina-l-kufri wa-l-faqr, wa aʿūdhu bika min ʿadhābi-l-qabr, lā ilāha illā Ant.
Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya mwili wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya usikizi wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya uoni wangu, hapana Mola asae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, (mara tatu). Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe. (mara tatu).
— (Abū Dāwūd 5090, Aḥmad 20430)
Hisia na dua zinazohusiana
Hisia mara nyingi huingiliana. Mkusanyiko huu wa karibu unaweza kueleza hali yako kwa usahihi zaidi.